Jumatatu 15 Septemba 2025 - 00:16
Hukumu za Kisheria | Kuwatazama wanawake wenye ulemavu wa akili wasiokuwa na hijabu ya kutosha

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Khamenei amejibu istiftaa kuhusiana na hukumu ya kuwatazama wanawake wenye ulemavu wa akili ambao hawana mavazi ya kutosha na kamili.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika jamii ya kibinadamu kuna watu wanaoishi katika hali na mazingira mbalimbali. Sheria za Kiislamu, zikiwa ni mpango kamili wa maisha, zimeweka mwongozo wa kudhibiti mahusiano ya binadamu katika nyanja zote, miongoni mwa masuala muhimu ya kisheria na kijamii ni suala la kutazama na mipaka yake katika uhusiano na wasio mahram, jambo linaloathiri moja kwa moja usalama wa mahusiano ya mtu binafsi na kijamii.

Miongoni mwa masuala mahsusi katika uwanja huu ni namna ya kuamiliana na hasa kuwatazama wanawake wenye ulemavu wa akili (upungufu wa akili). Watu hawa, kutokana na hali zao za kiakili, huenda wasiwe na ufahamu kamili wa hukumu za kisheria kama vile ulazima wa kuwa na hijabu kamili, kwa sababu mbalimbali, wakati mwingine wanaweza kutokuwa na mavazi ya kutosha yanayokubaliana na vigezo vya kisheria, Hali hii huibua maswali muhimu ya kifiqhi: Je, hukumu ya kuwatazama wanawake hawa, kutokana na hali yao maalumu, ni tofauti na hukumu ya wanawake wengine wasio mahram?

Mtukufu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amejibu istiftaa hii, na jibu lake linawasilishwa kama ifuatavyo.

Swali:
Ni ipi hukumu ya kuwatazama wanawake wenye ulemavu wa akili ambao hawana vazi la kutosha na kamili?

Jawabu:
Katika hukumu ya kuwatazama wasio mahram, hakuna tofauti kati ya wanawake hao waliotajwa na wanawake wengine.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha